• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Halmashauri ya Mji Njombe Yamwaga Samani kwa Shule za Sekondari

Tarehe iliyowekwa: June 11th, 2020

Halmashauri ya Mji Njombe imekabidhi meza na viti 280 vyenye thamani ya Shilingi milioni ishirini na tatu laki mbili na elfu arobaini kwa ajili ya Shule 4 za Sekondari zilizopo katika Halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wakati wa makabidhiano hayo Afisa Elimu Sekondari Rehema Nswila amesema kuwa Halmashauri kupitia mapato ya ndani ilitenga kiasi cha Shilingi milioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa meza, viti, vitanda kwa ajili ya kutatua changamoto katika Shule za Sekondari zilizokuwa na uhitaji.

“Wote tunatambua jitihada kubwa alizozifanya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika sekta ya elimu.Elimu bila malipo imepelekea kuwepo na ongezeko kubwa la Wanafunzi katika Shule zetu. Na sisi kama Halmashauri tupo kwenye mapambano ya kuhakikisha kuwa kila Mwanafunzi anapata Elimu bora ikiwa ni sambamba na kupata mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.Kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri tunakabidhi meza na viti 280. Tuhakikishe kuwa Wanafunzi hawafanyi uharibifu na zinatumika vyema.” Alisema

Editha John Mkuu wa Shule ya Sekondari Yakobi, Alex Chengula Shule ya Sekondari Uwemba, James Tamaa Mbele na Alex Tchwodzie kutoka Shule ya Sekondari Luhololo wameishukuru Halmashauri kwa kuwapatia samani hizo ambazo zitasaidia kutatua changamoto iliyokuwepo kwa kiasi kikubwa.

“Shule ya Sekondari Luhololo kwa sasa tunakamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na sasa tumepata madawati na meza themanini, yatakayoenda kuwekwa kwenye madarasa hayo. Badala ya Wananchi kuchangia meza na madawati tutaendelea na miradi mingine kwani Halmashauri imeshatusogeza. Alisema Mwalimu Alex

Halmashauri ya Mji Njombe kupitia mapato ya ndani imekabidhi madawati na meza 80 kwa Shule ya Sekondari Uwemba, Yakobi  na Luhololo na madawati na meza 40 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mgola na hivyo kufanya idadi yake kuwa 280.






Matangazo

  • MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021,SHULE ZA KITAIFA, TEULE NA KUTWA WANAFUNZI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 18, 2020
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021, SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 15, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Mvua yaleta maafa kwa familia 6 katika Kijiji cha Ikisa

    January 16, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe Yashika Nafasi ya Nne Matokeo Kidato cha Nne

    January 15, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe yatoa taulo za kike kwa Shule za Sekondari

    January 07, 2021
  • Jafo afurahishwa ujenzi wa Vituo vya Afya Njombe Mji

    December 22, 2020
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe