• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Halmashauri ya Mji Njombe yatoa taulo za kike kwa Shule za Sekondari

Tarehe iliyowekwa: January 7th, 2021

Halmashauri ya Mji Njombe imeweza kutekeleza kikamilifu agizo la Serikali kwa kuzitaka Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa taulo za kike ambapo kiasi cha shilingi milioni kumi kiliweza kutumika kwa ajili ya ununuzi wa taulo hizo kwa Shule za Sekondari.

“Kwa kuanza Halmashauri imeweza kutenga kiasi cha Shilingi milioni kumi ambapo  Halmashauri imeweza kununua maboksi 260 ambapo kila boksi lina paketi 24 na kufanya jumla ya taulo sitini na mbili elfu na mia nne ambazo zitagawiwa kwa Shule zote 24 zenye wanafunzi wa kike katika Halmashauri ya Mji Njombe.” Alisema mratibu wa mpango ngazi ya Halmashauri Joyce Ngata.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano kwa wanafunzi wa kike Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri amesema kuwa kwa sasa taulo za kike limekuwa si jambo la aibu kama ilivyokuwa zamani na imekuwa ni sehemu ya usafi kwa mtoto wa kike na ameipongeza Halmashauri kwa kutekeleza maagizo hayo.

 “Serikali pia imeweza kuliwekea mkazo na Halmashauri imeweza kulitekeleza kwa kasi kubwa. Hii ikawe ni utunzaji bora wa afya za  wanafunzi wa kike  waelekezwe namna nzuri ya uhifadhi mara baada ya matumizi ili zisisababishe uchafuzi wa mazingira.”Alisema Mkuu wa Wilaya

Aliendelea kusema “Tuwasaidie watoto wakike wasiweze kupoteza masomo. Kuna kipindi watoto wa kike wanashindwa kwenda shuleni kwa kukosa hifadhi nzuri.

Kwa upande wake Mkuu wa  Shule ya Sekondari Mbeyela Valeno Kitalika amesema kuwa Taulo hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa Wanafunzi wa kike kwani kuna wazazi wanoshindwa kumudu gharama za kununua vifaa hivyo kupelekea watoto wa kike  kushindwa kuhudhuria shuleni katika kipindi wawapo katika mizunguko yao.

Wakipokea taulo hizo baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Agness Trust Tumaini Maheve na Sayuni Festo Mhagama kutoka Shule ya Sekondari Maheve wamesema kuwa taulo hizo zitawasaidia kuweza kuhudhuria vipindi vyote vya darasani  na kuwafanya kuwa huru zaidi.

Halmashauri inaendelea na utaratibu wa kutenga fedha na kuhakikisha kuwa katika kila mwaka taulo za kike zinanunuliwa kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya Msingi mpaka Sekondari.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021,SHULE ZA KITAIFA, TEULE NA KUTWA WANAFUNZI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 18, 2020
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021, SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 15, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Mvua yaleta maafa kwa familia 6 katika Kijiji cha Ikisa

    January 16, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe Yashika Nafasi ya Nne Matokeo Kidato cha Nne

    January 15, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe yatoa taulo za kike kwa Shule za Sekondari

    January 07, 2021
  • Jafo afurahishwa ujenzi wa Vituo vya Afya Njombe Mji

    December 22, 2020
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe