• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Maandalizi ya kuhamia Soko jipya Njombe yaanza

Tarehe iliyowekwa: December 12th, 2020

Halmashauri ya Mji Njombe imeanza vikao vya awali ikihusisha Wadau wa Maendeleo na Wafanyabiashara kutoka soko la Dodoma lengo ikiwa ni kupata maoni  ya utaratibu wa kurejea  katika Soko jipya ambalo ujenzi wake umekamilika.

Akizungumza wakati kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema kuwa vikao vya wadau na Wafanyabiashara juu ya ufunguzi wa soko jipya ni muhimu kwani vitasaidia kupata mawazo chanya yatakayoleta maendeleo na pia kurahisisha utendaji kazi kwa usahihi katika soko hilo.

“Mawazo tutakayopata yatasaidia katika kuboresha Ufunguzi wa soko jipya la Njombe. Inabidi tutambue kuwa uwepo wa soko utawezesha kuboresha maisha na pia litasaidia kukuza sekta nyingine na ni vyema wafanyabiashara kutumia soko la Njombe kukuza biashara zao.Wapo wanaobeza mchakato wa uanzaji wa soko kuwa  taratibu hazikufuatwa.Naomba niwatoe shaka taratibu zote zitafuatwa kwa kadri ya makubaliano ambayo tutakuwa tumeyaafiki pande zote ”Alisema Mkuu wa Wilaya.

Bi Ruth amesema kuwa kuwa mpango wa uendeshaji wa huduma za soko ni kuhakikisha kuwa huduma inapatikana kwa masaa 24 tofauti na hali ya sasa ambapo mwisho ni saa kumi na mbili nusu jioni na hivyo kuwataka wafanyabiashara kujiandaa kwa hilo.

Akiwasilisha taarifa ya soko kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mji Njombe Afisa Mifugo wa Halmashauri Thadei Luoga amesema kuwa Halmashauri imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa tarehe 20/12/2020 awamu ya kwanza ya wafanyabiashara inaanza kuingia sokoni ikifuatiwa na awamu ya pili tarehe 23 na uzinduzi wa soko utafanyika kwenye mkesha wa mwaka mpya.

Kwa upande wao Wadau wa Maendeleo na Wafanyabiashara wameipongeza Halmashauri kwa kazi kubwa ya kusimamia na kukamilika kwa soko jipya na wameomba Halmashauri ihakikishe kuwa utaratibu unafuatwa ili wafanyabiashara waweze kurudi kuendelea na shughuli zao bila ya upendeleo wa aina yoyote.

“Tunaomba katika soko jipya wafanyabiashara waelimishwe juu ya kutumia mizani, matumizi ya vifaa vya kielektroniki kwenye mabucha, usafi na usimamizi mzuri ndani ya soko. Pia tuhakikishe kuwa usafiri na ulinzi ni wa uhakikika muda wote ili soko liweze kufanya kazi masaa 24. Alisema mmoja wa wadau

Kwa sasa Halmashauri imehitimisha zoezi la kutoa fomu za maombi kwa Wafanyabiashara watakaopenda kufanya biashara katika soko jipya zoezi lililohitimishwa tarehe 11/12/2020 ambapo idadi kubwa ya Wananchi imejitokeza kufanya  maombi.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021,SHULE ZA KITAIFA, TEULE NA KUTWA WANAFUNZI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 18, 2020
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021, SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 15, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Mvua yaleta maafa kwa familia 6 katika Kijiji cha Ikisa

    January 16, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe Yashika Nafasi ya Nne Matokeo Kidato cha Nne

    January 15, 2021
  • Halmashauri ya Mji Njombe yatoa taulo za kike kwa Shule za Sekondari

    January 07, 2021
  • Jafo afurahishwa ujenzi wa Vituo vya Afya Njombe Mji

    December 22, 2020
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe