• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Waziri Mkuu azitaka Halmashauri zenye kilimo cha Chai kuanzisha vitalu vya miche

Tarehe iliyowekwa: March 10th, 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote zinazolima zao la chai kuanzisha vitalu vya miche ya chai na wakulima kupatiwa bure bila malipo ili kuinua uzalishaji wa zao hilo nchi.

Hayo yalisemwa wakati wa kufungua kikao cha wadau wa zao la chai kilichofanyika katika Mkoa wa Njombe kikilenga  kujadili mwenendo wa uzalishaji zao hilo ambapo kuanzia mwaka 2018 uzalishaji wake umeonekana kushuka.

“Kila Halmashuari ianzishe kitalu cha ekari tatu na kuotesha miche bora ya chai na iwapatie Wananchi.Kazi hii ifanyike kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri”Alisema Waziri Majaliwa

Kwa sasa zao la chai linalimwa katika Wilaya 12 zilizopo kwenye mikoa sita ambayo ni Mbeya, Njombe, Iringa, Tanga, Kagera na Kilimanjaro. Jumla ya eneo lililopandwa chai ni hekta 22,721 ambapo wakulima wakubwa wana hekta 11,272 na wakulima wadogo hekta 11,449.

Akizungumzia kuhusu madai ya Wakulima wa chai Waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa wamiliki wa kampuni ya DL inayomiliki viwanda vya Chai Ikanga, Luponde na Itona kuwalipa wakulima wadogo wa chai madai yao ya fedha kufuatia kuuza majani mabichi ya chai kwa muda mrefu bila malipo.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo  Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema lipo suala la ucheleweshwaji wa malipo linalofanywa na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya chai jambo ambapo halikubaliki na kuwataka  wawekezaji wote wawalipe wakulima fedha zao kwa wakati.

Waziri wa Kilimo amesema ifikapo mwezi Mei mwaka huu wanatarajia kufungua mnada wa kuuza chai jijini Dar es Salaam hali itakayosaidia kupatikana kwa soko la uhakika.

 Mwenyekiti wa vikao vya wadau wa chai, Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda ameiomba Serikali kuiwezesha Bodi ya Chai Tanzania (TBT) na Taasisi ya Utafiti wa zao la Chai (TRIT) kwa kuipatia vitendea kazi na wataalamu ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.Dhamira ya Serikali ni kuona zao hilo linapata mafanikio, hivyo amewataka watendaji wafuatilie kuhakikisha wakulima wote wananufaika na zao hilo.

 

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021,SHULE ZA KITAIFA, TEULE NA KUTWA WANAFUNZI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 18, 2020
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021, SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE December 15, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Halmashauri ya Mji Njombe yatoa Milioni 239 ya mikopo katika robo ya tatu

    April 16, 2021
  • Mkuu wa Wilaya ya Njombe awatoa hofu Watumishi.Awataka kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa uzalendo,ujasiri na uthubutu

    April 01, 2021
  • Watumishi Halmashauri ya Mji Njombe wapatiwa mafunzo utambuzi noti bandia na utunzaji fedha

    March 16, 2021
  • "Parachichi ni Pesa" Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ateta na Wakulima

    March 12, 2021
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe