TARATIBU NA VIGEZO VYA KUPATA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI ITOLEWAYO NA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE
• Kikundi lazima kisajiliwe kama kikundi cha wanawake au vijana
• Kikundi cha wanawake au vijana kiwe kinajishughulisha na ujasiliamali au kinakusudia kuanzisha shughuli za ujasilamali mdogo au wa kati
• Kwa kikundi cha wanawake au vijana kiwe na idadi ya wanakikundi kuanzia watano na kuendelea
• Kikundi cha wanawake au vijana lazima kiwe na akaunti ya benki ya iliyofunguliwa kwa jina la kikundi na kwa ajili ya matumizi ya kikundi.
• Kikundi cha wanawake/vijana lazima wawe raia wa Tanzania wenye akili timamu na umri wa miaka 18 na kuendelea.
• Kwa vikundi vya vijana lazima umri uzingatiwe kuanzia miaka 18 na ukomo wake ni miaka 35.
• Wanufaika wa mikopo hii ni wale wasio na ajira rasmi.
• Vikundi vyote lazima viwe na barua toka kwa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kwamba kikundi husika anakitambua kwa upana na miradi ya kikundi ilipo.
• Kikundi cha wanawake/vijana wanaojishughulisha na biashara lazima wawe na leseni ya kikundi.
• Kikundi cha wanawake/vijana lazima kila mwanachama awe na kitambulisho cha NIDA
• Kundi hili linaweza kukopeshwa kikundi au mtu mmoja,endepo Kamati ya kudumu ya Fedha,Mipango na Uongozi itajiridhisha kuwa mtu huyo amekosa mtu mwingine mwenye ulemavu na sifa ya kuwa mwanakikundi wa kikundi cha watu wenye ulemavu.
• Anajishughulisha na ujasiriamali au anakusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati.
• Mlemavu lazima awe na akaunti benki yenye jina lake halisi kwa matumizi yake ya kijasiriamali
• Awe raia wa Tanzania mwenye akili timamu na umri wa miaka 18 na kuendelea.
• Wanufaika wa mikopo hii ni wale wasio na ajira rasmi.
• Kwa mtu mmoja mlemavu anayeomba mkopo lazima awe na cheti cha kuzaliwa.
• Kwa kikundi/Mlemavu mmoja lazima kuwa na barua toka kwa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kwamba kikundi husika anakitambua kwa upana na miradi ya kikundi ilipo.
• Kikundi cha watu wenye ulemavu/Mtu mwenye ulemavu anayejishughulisha na biashara lazima wawe na Leseni ya biashara
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe