HAMASA YATOLEWA NJOMBE TC KWA SHULE ZA SEKONDARI KUFANYA VIZURI ZAIDI MITIHANI YA KIDATO CHA NNE.
Hamasa hiyo imetolewa tarehe 16.Mei.2023 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji NJOMBE Mhe.Erasto Mpete Wakati akikabidhi zawadi kwa shule mbili za Sekondari zilizoongeza ufaulu na kufanikiwa kuondoa sifuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2022.
Halmashauri ya Mji NJOMBE Kupitia Mkurungenzi wake Mhe Kuruthumu Sadick Imetekeleza ahadi yake ya kutoa zawadi kwa shule zinazofanya vizuri kwa mitihani ya kidato cha nne katika operesheni ya tokomeza sifuri.
Miongoni mwa shule zilizopewa zawadi Tarehe 16/05/2023 ni shule ya sekondari Luholola na Shule ya Sekondari Mgola ikiwa ni utekelezaji wa makubalio yaliyofanyika katika siku ya wadau wa Elimu
Akizungumza kwa Niaba ya Mkurungenzi wa Halmashauri ya Mji, kaimu Mkurungenzi Ester Gama amesema" tumeweza kutekeleza agizo ambalo lilitolewa katika kikao cha wadau wa elimu kuutambua mchango wa watumishin wanapofanya vizuri katika kazi na inaongeza hamasa zaidi katika ufundishaji".
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe ametumia fursa hiyo kuzipongeza shule hizo kwa kuongeza ufaulu na kufanikisha kufuta sifuri akieleza siyo kazi rahisi na zawadi hiyo itumike kama motisha kufanya vizuri Zaidi katika mtihani ijayo kwa shule Zote za sekondari ili kuiweka halmashauri katika Nafasi nzuri kiufaulu.
Naye Prochesusi Mguli Afisa Elimu Sekondari ameseme kutolewa kwa zawadi hizo nikutambua mchango mkubwa wa walimu ambao wanaufanya katika kuhakikisha taaluma inakuwa kwa kasi na kudhamini mchango wao katika utendaji wa kazi.
Wakizungumza baada yakukabidhiwa zawadi hizo wakuu wa shule hizo mbili,Shule ya Sekondari Luholola na Shule ya Sekondari Mgola wemeushukuru uongozi wa halmashauri kwa kutekeleza ahadi hiyo nakusema hiyo ni motisha kwao na kwa waalimu wengine kujibidisha ili kufanya vizuri Zaidi.
"NI furaha kwangu kama mkuu wa shule. Kwa shule yangu hii ni Mara ya kwanza kupokea zawadi hii tangu kuanza kutolewa, ni mwanzo mzuri na motisha kwetu Kuendelea kufanya vizuri." Amesema Mkuu wa Shule ya Sekondari Luhololo Mwalimu
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Mgola Mwalimu Mfungilwa Amesema pamoja na Kutokomeza sifuri katika Shule yake wamefanikiwa kuongeza ufaulu kwa kupata division one ya alama saba (7) Zaidi ya moja. Ameongeza kuwa siyo Mara Yao ya kwanza kwa shule hiyo kupokea zawadi hiyo Inaenda kuongeza hamasa na nguvu kwa waalimu kujituma Zaidi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe