• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI (LAAC) YAKAGUA MRADI WA STENDI NA SOKO NJOMBE

Tarehe iliyowekwa: March 17th, 2022

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imekagua na kutembelea katika Stendi ya Mabasi Njombe na Soko Kuu Njombe lengo ikiwa ni kujiridhisha na utekelezaji wa matumizi ya fedha zilizotengwa kwenye miradi hiyo.

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (LAAC) Grace Tendega amesema kuwa licha ya kuwa Kamati hiyo inalengo la kuangalia ni kwa namna gani fedha zilizotengwa kwenye miradi zinatumika lakini pia kamati inalengo la kuhakikisha kuwa kero zilizopo kwenye utekelezaji wa miradi hiyo zinapatiwa ufumbuzi kwa kufanya utatuzi  na hivyo kufanya miradi iliyokusudiwa na Serikali kwa Wananchi kuwa endelevu na kuwa na tija kwa Wananchi.

 Akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa Stendi na Soko Afisa Mipango wa Halmashauri Shigela Ganja amesema kuwa Halmashauri ya Mji Njombe imefanikisha utekelezaji wa Ujenzi wa Stendi na Soko kupitia Programu ya Uimarishaji na Uboreshaji Miji (ULGSP) na hivyo kufanikiwa kupata kiasi cha Shilingi Bilioni 20 ikiwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo jambo ambalo liliepusha Halmashauri kuendelea na wazo na kukopo kwenye taasisi za kifedha ambazo pengine zingeweza kuwa na riba kubwa kwenye urejeshaji wa mkopo huo.

 Aidha Ganja amesema kuwa licha ya kuwa Mradi wa Stendi na soko imebadili mandhari ya Mji na kuwezesha mazingira bora ya kutolea huduma, bado changamoto ya utekelezaji wa mradi wa stendi umeshindwa kuzaa matunda yaliyokusudiwa kutokana na kuwepo na stendi katikati ya Mji jambo linalopelekea abiri wengi kuishia mjini na stendi kushindwa kufanya kazi na kukusanya kwa kadri ya malengo Halmashauri iliyojiwekea.

 Changamoto hiyo ya ufanisi wa stendi ukawaibuwa Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamatai hiyo kuoneshwa kutoridhishwa kwao na utendaji wa stendi hiyo ikiwemo idadi ya mabasi, Wananchi wanaotumia stendi hiyo na vibanda kushindwa kukodishwa .

 Akizungumza katika kikao cha majumuisho mara baada ya kutembelea na kukagua miradi ya stendi na soko kuu ambayo miradi hiyo imeanza kutumika Mwenyekiti wa Kamati hiyo Grace ametoa maelekezo kwa Halmashauri kuhakikisha kuwa viongozi kwa kushirikiana na Halmashauri unakubaliana kutotumia stendi ya mabasi iliyopo mjini kwani inahatarisha usalama wa abiria na Wananchi na inaweza kusababisha maafa kwani stendi hiyo ipo kwenye hifadhi ya barabara na katikati ya Mji.

“Halmashauri mhakikishe kuwa katika katika maeneo yenye kasoro za ujenzi zikiwemo nyufa kwenye barabara za magari makubwa stendi kuu , na sakafu katika jengo la mama ntilie zinarekebishwa kufikia mwezi Juni. Aidha Mhamasishe  Wafanyabiashara kupanga katika fremu za maduka  zilizosalia na kufanya marekebisho katika soko la Dodoma ili wafanyabiashara wengine waweze kuhamishiwa huko na tuweze kupunguza msongamano katika soko jipya.”Alisema Mwenyekiti

 Aliendelea kusema “Kumekuwa na majanga ya moto katika masoko mengi katika siku za hivi karibuni. Niwaombe muhakikishe kuwa soko linakuwa na Bima na pia  kuboresha miundombinu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu katika soko kuu hususani kwenye huduma ya migahawa.”Alisema Grace

 Licha ya changamoto hizo na mapendekezo kamati hiyo pia imetoa pongezi kwa Watendaji kwa kuweza kufanya utekelezaji wa miradi na pia imeishauri Halmashauri na Wataalamu kuendelea kuwa Wabunifu wa vyanzo vya mapato na pia kuhakikisha kuwa mashine za kukusanyia mapato zinatumika katika maeneo ya makusanyo.

  Katika hatua nyingine Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Ally Mwinyi akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya stendi mpya ya Njombe, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi hakipo tayari kuona Mwananchi akionewa na Halmashauri ikipoteza mapato kwani Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa stendi mpya ya kisasa na kuelekeza matumizi ya stendi yaendelee kama ilivyokuwa wakati stendi ikiwa inaanza  kwa kufuta kituo cha msaada cha sasa kilichopo stendi ya zamani na badala yake kutumia stendi kuu na vituo vilivyokuwa vimeainishwa vya Nundu,Kibena,Ramadhani na stendi mpya.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 06, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWENYE ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE March 25, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DC AFURAHISHWA NA MWENENDO WA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATA YA MATOLA

    June 10, 2022
  • ZIARA YA DC KISSA YAWAIBUA WANANCHI KUPATA CHANJO YA UVIKO

    June 09, 2022
  • DC NJOMBE AIELEKEZA IDARA YA ARDHI KUSHUGHULIKIA MGOGORO WA ARDHI NDANI YA WIKI MBILI

    June 08, 2022
  • DC NJOMBE AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI NA KUPIGA MARUFUKU UENDELEZAJI VYANZO VYA MAJI

    June 05, 2022
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe