Tunawakaribisha watanzania wote kwenye Banda la Halmashauri ya Mji Njombe .
Karibuni Mjifunze ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kibiashara ,Ng'ombe wa Nyama kibiashara,Uzalishaji wa Vifaranga vya samaki na ufugaji wa samaki kwenye mabwawa,Ufugaji wa kuku wa Mayai kibiashara,Kilimo cha mbogamboga kwenye kitalu nyumba,ufugaji wa Nyuki na uvunaji wa mazao yatokanayo na Nyuki,kilimo cha parachichi na viazi mviringo.Yapo Mengi yakujifunza kwenye sekta ya Kilimo mifugo na Uvuvi.
Karibu upate uzoefu na mbinu mbalimbali za ujasiriamali .
Wataalamu, wakulima na wajasiriamali mbalimbali watakuwepo kukuhudumia kwenye banda letu la maonesho katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya kuanzia Agosti 1 - 8 ,2024.
Usikose fursa hii adhimu yakujifunza.
"Chagua Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe