Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu ,ili tuweze kunufaika na sekta hii muhimu inatupasa kujifunza nakuongeza ujuzi kila wakati .
Nitumie fursa hii kuwakarihisha katika Maonesho ya wakulima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayoendelea Jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale kwa ajili ya kubadilishana maarifa, teknolojia na mbinu bora za kilimo ambazo zitasaidia kuboresha uzalishaji na kipato cha wakulima wetu.
Karibuni kwa wingi katika banda la Halmashauri ya Mji Njombe ili kupata fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalamu mbalimbali na wakulima wazoefu pia kuona bidhaa mpya na huduma zinazopatikana kwenye sekta ya kilimo mifugo na Uvuvi.
Ninawahimiza wananchi wote wa Jimbo la Njombe Mjini kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na maonesho haya muhimu.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe