Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Godfrey Mnzava baada ya ukaguzi wa miundombinu na nyaraka amefanya uzinduzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya mji Njombe (Kibena).
Mradi huo umegharimu jumla ya fedha shilingi 173,333,350.00 ambapo kiasi cha shilingi 150,055,000.00 ni fedha kutoka Serikali kuu(TASAF), 16,342,000.00 ni Mapato ya ndani ya Halmashauri, 3,570,000.00 michango ya Wananchi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Njombe ilifanya harambee na kupatikana kiasi cha shilingi 3,200,000.00.
Lengo la Mradi huo ulioibuliwa na wananchi ni kuboresha mazingira ya Wodi ya akina mama ambayo awali hayakuwa mazuri kwa afya na ustawi wa mama na mtoto wakati wa kujifungua hususani watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti).
Takwimu zinaonyesha kuwa tangu huduma zianze kutolewa mwezi Januari 2024, Jumla ya wakimama 1069, watoto wachanga 1046 na watoto njiti 53 wamepatiwa huduma.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 zinaongozwa na kaulimbiu isemayo "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe