Akizungumza Julai 17,2024 Ndg.Godfrey Mnzava mkimbiza Mwenge Kitaifa 2024 na wananchi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali baada kukagua na kusikiliza wimbo kutoka Klabu ya kupambana na Rushwa iliyopo Shule ya Sekondari Mpechi katika ameitaka jamii kuhakikisha inajenga tabia ya uzalendo katika utekelezaji wa miradi ya Serikali na kutoa taarifa ya vitendo viovu au viashiria vinavyo sababisha rushwa katika jamii jambo ambalo hupelekea husababisha madhadhara.
“Leo hii tumeshuhudia wanafunzi hawa wakitufundisha kwa kutumia wimbo wa kuzia Rushwa katika jamii,niombe viongozi wa Serikali na wananchi mlio jitokeza katika eneo hili tuwe mabalozi wa zuri wa kutoa taarifa vitendo vyote viovu vinavyo vyenye viashira vya rushwa katika jamii ,tukifanya hivyo basi tutakuwa na jamii bora ” Ndg.Godfrey Mnzavana Mkimbiza Mwenge Kitaifa 2024
Aidha amweomba Walimu wanao simamia klabu za rushwa shuleni kuhakikisha wanasimamia kikamilifu klabu hizo ili ziweze kuleta maendeleo Chanya katika jamii.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zinaongozwa na kaulimbiu isemayo "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
@kissagwakisakasongwa @njombe_rs
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe