Tarehe 14 Februari 2025, Halmashauri ya Mji Njombe imetoa taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Jumla ya wanafunzi wa kike 8,554 watanufaika na taulo hizo ambazo zimatajwa kusaidia kupunguza utoro shuleni na kuwaondolea hofu wanapokuwa kwenye hedhi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe, Mhe. Erasto Mpete, ameongoza ugawaji wa taulo hizo, ambapo shilingi milioni 10 zilitumika kununua taulo za kike kwa wanafunzi 6,874 wa shule za sekondari, huku shilingi milioni 5 zikitumika kununua taulo kwa wanafunzi 1,680 wa shule za msingi.
Mhe. Mpete ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick kwa kuwa na maono hayo kwa ajili ya watoto wa kike na kuendelea kuyatekeleza kila mwaka kama ilivyo kwenye mpango na bajeti ya halmashauri.
Mpango huu unalenga kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwepo katika elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa kike.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe