• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

ZIARA YA DC KISSA YAWAIBUA WANANCHI KUPATA CHANJO YA UVIKO

Tarehe iliyowekwa: June 9th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mheshimiwa Kissa Gwakisa Kasongwa amewataka Wananchi wa Kijiji cha Boimanda Kata ya Matola kuacha habari za upotoshaji juu  ya matumizi ya  chanjo ya UVIKO 19 ambapo Wananchi wengi wamekuwa na imani potofu juu ya matumizi ya chanjo hiyo.Akizungumza wakati wa ziara yake katika    Kijiji cha Boimanda Kata ya Matola Halmashauri ya Mji Njombe

 Mheshimiwa Kissa amewataka Wananchi kupuuza habari za mitandao na za uzushi kuwa chanjo ya UVIKO inaleta madhara kwenye afya na kupelekea kifo na pia kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.“Ingekuwa chanjo ya UVIKO Inamadhara basi Mheshimiwa Rais angekuwa wa kwanza kupata madhara hayo kwani ndiye aliyeongoza zoezi la utoaji chanjo.Mimi mwenyewe nimechanja na mpaka sasa bado nipo vizuri.Tungetaka kuuliwa tungeweza kuuliwa kwa njia mbalimbali,yapo mambo mengi tunapokea kutoka nje ya nchi.Na huduma ya chanjo haijaanza leo ni huduma ya siku nyingi.Ukiona mtu anaongea maneno ya uongo juu ya chanjo basi huyo ujue hayajamkuta. Tujitokeze kuchanja, Chanjo ni salama na ni kwa ajili ya uhai wetu.”Alisema Mkuu wa Wilaya.

Wakizungumza mara baada ya kusikiliza elimu ya chanjo waliyopatiwa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya baadhi ya Wananchi kutoka katika Kata ya Matola Kijiji cha Boimanda wameshukuru ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya kwani imewapa hamasa kwao kushiriki zoezi la chanjo kwani uelewa juu ya uchanjaji ulikuwa ni mdogo.Winfrida Joseph Mgaya na Elizabeth John ni wakazi wa Kijiji cha Boimanda ambao kwa pamoja wanamshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa elimu hiyo ambayo iliwapelekea kupatiwa huduma ya chanjo.“Mwanzoni nilikua sielewi maana walisema kuwa chanjo zinamadhara na wakati mwingine zinaweza kusababisha kifo lakini nashukuru leo nimepata elimu na nimechanja. Nawashauri wenzangu ambao bado hawajachanja kuhakikisha kuwa wanachanja”Alisema Elizabeth.

Licha ya kutoa elimu ya chanjo na kutoa jumbe kuu za Serikali ikiwa ni Pamoja na suala la sensa na mbolea Mkuu wa Wilaya pia amebahatika kutembelea katika shule ya Msingi Boimanda na kujionea hali halisi ya madarsasa ambapo ameshauri kuwa Halmashauri ione ni kwa namna gani inaweza kutenga fedha kupitia zidio la makusanyo ili kujenga vyumba vipya vya madarasa katika shule hiyo kutokana na uchakavu uliopo katika shule hiyo kwa sasa.Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe anaendelea na ziara yake ya kutembelea katika kila kijiji kuzungumza na wananchi na kutatua kero mbalimbali ambapo kwa leo yupo katika Katt ya Matola Halmashauri ya Mji Njombe.

Matangazo

  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA LUNYANYWI NA YAKOBI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE August 05, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWENYE ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE March 25, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 06, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DC KISSA AWATAKA WASHIRIKI NANE NANE KUTOKA WILAYA YA NJOMBE KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA JAMII NA KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO NJOMBE

    August 02, 2022
  • MAKAMU WA RAIS AMTEMBELEA MFUGAJI WA SAMAKI KWENYE UZINDUZI WA MAONESHO YA NANENANE

    August 01, 2022
  • MKOA WA NJOMBE WAFANYA KONGAMANO KUMWOMBEA MHESHIMIWA RAIS NA KULIOMBEA TAIFA AMANI

    July 30, 2022
  • UWEMBA NA NJOSS ZATOKOMEZA SIFURI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA.HALMASHAURI YATOA PONGEZI YA CHETI NA KITITA CHA LAKI TANO KWA KILA SHULE

    July 29, 2022
  • Angalia zote

Video

Makala ya utekelezaji miradi ya maendeleo 2020 Halmashauri ya Mji Njombe
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe