MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI
Kuelimisha jamii kushiriki katika mambo mbali mbali ya shule kupitia vikao vya mitaa ambavyo wananchi watahudhuria na kutoa maoni.
Kuandaa bajeti ya idara na vitengo vyake ikiwa ni pamoja na mpango kazi unaoendana na bajeti hiyo.
Kusimamia na kuendeleza taaluma katika Halmashauri ya Mji Njombe kwa kusimamia ufundishaji, ujifunzaji mahudhurio ya walimu,
wanafunzi na utendaji kazi kwa ujumla.
Kuandaa takwimu mbalimbali za kielimu za wanafunzi, walimu, samani na miundombinu.
Kuratibu mashindano ya taaluma na michezo kwa shule za msingi.
Kusimamia haki na maslahi ya walimu kwa kufuata taratibu kama vile ruhusa, likizo masomo, matibabu n.k.
Kuhudumia jamii kuhusiana na mambo yote ya kielimu na mafunzo mbalimbali kupitia kamati za shule na shuguli
nyinginezo kama vile uhamisho wa wanafunzi.
Kuandaa na kuendesha vikao mbalimbali vya wadau wa elimu katika ngazi zote za Halmashauri.
Kuandaa Tange ya walimu wa shule za msingi kwa kila mwaka.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe