Mhe.Mwanaidi Ali Khamis Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalumu amepongeza kikundi cha Twaweza Kilichopo Kata ya Mji mwema Halmshauri ya Mji Njombe kwa kutumia Fursa za Mikopo ya asilimia 10 ambayo inatolewa na Halmashauri .
Naibu waziri ametoa Pongezi hizo Julai 05,2024 alipotembelea eneo la uzalishaji la kikundi cha Twaweza ambacho kinazalisha bidhaa mbalimbli za Ushonaji jambo ambalo limepelekea kuzalishwa kwa ajira nyingine ambazo zimetokana na mkopo huo ambao walipewa na Halmashauri .
"Tumezoea kuyaona mambo haya China lakini kwa juhudi za Serikali tunayaona katika Nchi yetu niwapongeze vijana kwa uthubutu wenu wakufika na kujiunga na kikundi hiki na pia niombe vijana kuweni mabalozi wazuri kwa wale ambao bado hawazijuwi fursa hizi " Alisema Mhe.Mwanaidi Ali Khamis Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalumu.
Aidha Mhe Naibu waziri ameiomba Idara ya Maendeleo ya Jamii kuendelea kutoa elimu juu ya ujio wa mikopo ya asilimia kumi ambayo itatolewa na Halmashauri kupitia Benki.
Mkuu wa Wilaya Njombe Mhe. Kisa Gwakisa Kasongwa amempa siku nne mmiliki wa kampuni ya Chai ya DL Group kiwanda cha Luponde kuhakikisha analipa madai ya wafanyakazi wake wote ndani ya siku 4.
Ametoa agizo hilo Julai 02 ,2024 alipoyembelea kiwandani hapo nakuzunhumza na wananchi pamoja na wafanyakazi ambapo Mhe Kisaa Kasongwa kampuni hiyo haiwatendei haki watumishi wake kwani ni miezi minne wameganya kazi bila malipo.
“Nimekuja kuwasikiliza wananchi wangu ambao mmekuwa mkipaza sauti niombe muwe wavumilivu huku Serikali ikiwa inapambania maslahi yenu ,nampa siku 4 mmiliki wa kiwanda hiki kuhakikisha anawalipa wafanyakazi wake wote ambao wanawadai Pamoja na kuwalipa mafao yao ya NSSF” Alisema Mkuu wa Wilaya Njombe Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itakuja na suluhisho la kudumu kuhusu mwekezaji huyo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe