Waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa Njombe wameshauriwa kuiga mfano kwa kuweka kitengo maalum cha huduma kwa watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) katika hospitali za Wilaya kama ilivyo katika hospitali ya Mji Njombe (Kibena), ili kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Ushauri huo umetolewa Julai 1,2024 na Mkurugenzi wa huduma za Afya lishe na Ustawi wa Jamii akiwa ameambatana na timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) iliyofika hospitali mji wa Njombe(Kibena) ,kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya nakuona uwepo wa vyumba maalum vyenye vifaa vya kisasa kwa ajili yakuwahudumia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) na changamoto nyingine za afya.
Kitengo cha kuhudumia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) kipo ndani ya jengo la mama na mtoto lililojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 173.3 ,fedha iliuojumuisha michango ya wananchi ,fedha kutoka TASAF, fedha za mapato ya ndani na michango ya wadau wa maendeleo.
Mkurugenzi wa huduma za Afya lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Rashidi Mfaume Julai 1,2024 wakati wa Ziara ya ukaguzi wa huduma za Afya katika Halmashauri ya Mji Njombe ,ametoa pongezi kwa hospitali ya Mji wa Njombe(Kibena) kwa kuwa na kitengo cha mfano cha kuhudumia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu (Njiti) pamoja na usimamizi mzuri wa usafi wa mazingira uliowezesha hospitali hiyo kushika nafasi ya pili kwenye tuzo za usafi wa mazingira mwaka 2023.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe