Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Godfrey Mnzava ameagiza kuendelea kutolewa kwa elimu kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa ili wananchi wachague viongozi sahihi.
Ametoa maagizo hayo Tarehe 17,2024 wakati akizindua wimbo wa kutoa elimu na kuhamasisha uchaguzi wa Serikali za mitaa ulioandaliwa na kwaya ya REDEMED GOSPEL CHURCH pamoja nakuwapatia cheti kwaya hiyo iliyopo Mjini Njombe.
"Wananchi wakipata elimu itasaidia kujua ni kiongozi wa namna gani wanamtaka na watamchagua kwa sifa zile wanazoziona," amesema Mnzava,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024.
Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa katika Halmashauri ya mji zimemamilizika kwa wakimbiza mwenge kuridhia na kuzindua miradi 3 na kukagua miradi 3 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2,173,596,859.00.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe