Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Kuruthum Sadick, Aprili 11,2024 amezungumza na wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Yakobi na kuwatakia maandalizi mema ya mtihani wa taifa utakaofanyika kuanzia Mei 06,2024.
Bi. Kuruthum Sadick amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea kuwa na nidhamu nakujithamini kama mabinti nakukataa vishawishi vyovyote vitakavyowasababishia kupoteza mwelekeo na hatimaye kushindwa kutimiza ndoto zao.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe